
Shule ya sekondari ELIMIKA yenye namba ya usajili REG. S.5271 ni shule ya binafsi ya mchanganyiko ambayo imeanzishwa kwa makusudi ya kutoa Elimu Bora ya sekondari kwa watoto wa kike na kiume wanaopata nafasi ya kusoma katika shule hii.
Fomu za kujijunga na shule zinapatikana maeneo yafuatayo
- ELIMIKA SEKONDARI MJIMWEMA –SONGEA MJINI
- WILOLESI MEDICAL CLINIC –SONGEA MJINI
- MBEYA COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES –MBEYA
Shule itafanya usahilili wa kuwapokea wanafunzi wapya mnamo tarehe 10/11/2025, pia kwa wanaotaka kuhamiwa wanaruhusiwa mda wowote katika mwaka baada ya kufaulu usahili.
Kuna walimu makini na wenye uwezo wa kumpatia mtoto wako elimu bora na malezi mazuri. Shule hii iko Manispaa ya Songea, mtaa wa Mjimwema “B”
Masomo yote yanafundishwa katika lugha ya Kiingereza isipokuwa Kiswahili.
Wazazi wote walio na mategemeo makubwa kwa watoto wao kupata Elimu Bora na malezi mazuri na gharama zetu ni nafuu sana. Nyote mnakaribishwa. Usisubiri kuambiwa; njoo ujionee mwenyewe, waleteni watoto wajifunze.