Wilolesi Foundation inatarajia kuendesha mbio za hisani zitakazofanyika January 12, 2024 zitakazo julikana kama “Wilolesi Foundation Marathon” ikiwa na lengo la kuchangia ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya Watoto wachanga katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa Songea. Kauli mbiu yam bio hizi ni: “Kimbia kuokoa Maisha ya watoto wachanga”. Tukio hili litapata ufuatiliaji makini wa wadau mablimbali na hadhira kwa ujumla kupitia vyombo mbalimbali vya Habari kama runinga, redio, mitandao ya kijamii.

LENGO KUU

Kutoa msaada wa vifaa tiba kwaajili ya Watoto wachanga Hospaitali ya Rufaa ya Mkoa Songea.

Malengo Mahsusi

  1. Kuhimiza michezo ya kukimbia kwaajili ya kujenga afya mwili na akili.
  2. Kusaidia shirika na wadau kufikia malengo huku wakisaidia kukoa Maisha ya Watoto wachanga.
  3. Kuongeza kufahamiana na marafiki wapya
  4.  Kusheherekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar……..READ MORE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *